Jombi amuua mamake kwa kumpiga na jiwe

Hali tete na ya wasiwasi imetanda katika kitongojiduni cha Kibuku, kata ndogo ya Maragua kaunti ya Murang'a baada ya mwanamme kumuua mamake kwa kutumia jiwe. Kisa hiki kilifanyika jumapili jioni wakati wawili hawa walijipata katika cheche za majibizano.

Antony Mburu alimuua mamake kwa kumjeruhi vibaya na jiwe. Majirani wanakisia huenda matumizi ya dawa za kulevya yamechangia dogo huyu kumuua mamake.

Sarah Wambui, 53 ni mjane aliyejaliwa na watoto wanne. Mama huyu alifika kwake saa kumi na mbili akiwa na dadake na kumpata kijana wake pamoja na mjukuu.

Majibizano yalianza baada ya mama Anthony kutaka kujua ni kwa nini alichukua pikipiki kwa polisi na kuiendesha bila namba ya usajili. Mwanae alimweleza kuwa alikuwa amekubaliana na polisi aichukue.

Majibizano haya yalimkasirisha Anthony.

Mkuu wa polisi  eneo hilo Josphat Ondiri  amesema kuwa mshukiwa amekamatwa na uchunguzi umeanzishwa kubaini kilichofanya kijana huyu kumuua mamake.

Hadithi imehaririwa na kuchapishwa na Abraham Kivuva