José Filomeno dos Santos: Mwana wa aliyekuwa rais wa Angola's ahukumiwa miaka 5 gerezani

santos
santos

Mwana wa kiume wa aliyekuwa rais wa Angola amefungwa jela miaka mitano kwa udanganyifu alipokuwa anasimamia hazina ya ugenini ya nchi hiyo iliyo na utajiri mkubwa wa mafuta.

José Filomeno dos Santos, mwenye umri wa miaka 42, alishtumiwa kwa kujaribu kufuja hadi dola $1.5bn (£1.1bn) huku akiwa kileleni mwa hazina hiyo iliyokuwa na thamani ya dola bilioni tano kutoka mwaka 2013 hadi 2018.

Soma pia:

Alishtakiwa kwa kuiba dola milioni 500 kutoka hazina hiyo na kuhamishia pesa hizo kwa benki moja nchini Uswizi.

Babake Dos Santos', José Eduardo dos Santos, aliongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 38.

José Eduardo dos Santos alikuwa rais wa nchi hiyo kutoka mwaka 1979 hadi aliposjiuzulu mwaka 2017, na nafasi yake kuchukuliwa na jamaa aliyekuwa amemchagua yeye menyewe waziri wake wa zamani wa ulinzi Joao Lourenço.

Soma pia:

José Filomeno dos Santos, akijulikana sana kama Zenu, pia alikaa gerezani kwa kipindi cha miezi saba kuhusiana na tuhuma za ufisadi kabla ya kuachiliwa mwezi Machi.