Jovial in yellow

Otile hakuninunulia gari! Jovial amwambia Massawe Jappan

Jovial mmoja wa wanamziki wakubwa waonaochipukia alihojiwa na mtangazaji wetu Massawe Jappani.

Mwanamziki huyo kwa jina Juliet Miriam Ayub alizaliwa mjini Mombasa na amekuwa akipanda kimziki kwa kasi.

Massawe alimuuliza kuhusu gari analodaiwa kunununuliwa na Otile na akakanusha madai hayo akisema kwamba sio ya ukweli.

Massawe pia alimuuliza Jovial ni lini aligundua kuwa na kipawa cha kuimba.

Alisema kwamba alianzia uimbaji wake katika kanisa la kiangiliakana huko Mombasa.

Jovial in red
Jovial in red

Pia aliongeza kwamba alikuwa na mazoea ya kumwimbia babake ambaye alikuwa mcheza gita na mamake aliyekuwa muimbaji.

Jovial alieleza kwamba alikuwa na ari ya mziki maisha yake yote na kwamba alikuwa katika taaluma ya mziki kwa miaka tisa.

Massawe alimuuliza ni nini kilikuwa kimemuudhi sana katika mitandao ya kijamii? alijibu akisema “kulikuwa na watu waliokuwa wakimkera wakizungumza vibaya kuhusu mamake. Sikuwasaza. Heshimu wazazi wangu”.

Pia aliongeza kwamba anafanya kolabo nzito na msanii tajika.

Jovial aliulizwa kuhusu msanii anayemuenzi katika kanda ya Afrika mashariki na kati? Alisema anapenda Vanessa Mdee, Nandy na hata Sheba wa Uganda.

 

Nandy
Nandy

Alieleza kwamba wanamziki wa kike kutoka Kenya waliokatika mawazo yake ni Vivian na Nadia Mukami.

Mwanamziki huyo pia alimwabia Massawe kwamba yeye hutunza sana sauti yake kwa kunywa maji mengi yakiwa na ndimu na tangawizi.

Pia alisema anawaenzi sana wanamziki Diamond Platnumzi na Ali Kiba. Alisema Diamond anajua sana kujinadi.

TAARIFA IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO

kwa maelezo zaidi soma hapa

Photo Credits: Instagram

Read More:

Comments

comments