‘Jubilee ni kama karatasi, tutaitupa’ asema Oscar Sudi

Naibu wa rais William Ruto  na kambi yake huenda wanasalimu amri katika vita vya kukipigania chama cha Jubilee  ambacho awali alilenga kukitumia kuwania urais mwaka wa 2022 .

Washirika wake wamesema  walilenga kuiunganisha mirengo ya chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu ujao lakini kwa sababu kimetekwa na ‘walaghai  na mabroka’   hivi karibuni watatoa mwelekeo kwa wafuasi wao .

Hayo yamesema na mbunge Oscar Sudi  ambaye  amesema Ruto ana chaguo mbadala kuhusu chama atakachotumiwa kugombea urais .

"  Kama alivyosema bosi , tutajaribu kusuluhisha tofauti hizi  lakini tuna njia nyingine mbadala. Jubilee ni karatasi tu  na tutaibuka na karatasi nyingine wakati ufaao’ Sudi amesema

" Hata iwapo Ruto atawania urais kwa chama kiitwacho Sufuria  basi hapo ndipo tutakapoelekea’

Hata hivyo sudi amesema hatawakiacha Chama hicho bila kuwatoshoa kijasho wapinzani wao .

Sudi alikuwa akizungumza nyumbani kwake Eldoret  ambako alikuwa mwenyeji wa Zaidi ya waakilishi 69 wa kaunti kutoka   Uasin Gishu, Nandi  na  Trans Nzoia  kwa chakula cha mchana  na kujadili masuala ya eneo hilo.

Sudi amedai kwamba janga la covid 19 limeingizwa siasa  ili kuwazuia wafuasi wa Ruto kukongamana .

“ Nimekuwa nikizingumza kuhusu mambo mengi  likiwemo jambo hili feki la Covid 19 na hivi karibuni nitajitokeza kutabiri kitakachofanyika siku chache zijazo’ amesema Sudi

Sudi ameahidi kulipasha taifa  kuhusu mwelekeo  utakaochukuliwa na wafuasi wa DP Ruto .

Sudi alitangaza kwamba tazidi kuandaa hafla za mikutano na waakilishi wa kaunti kutoka   Baringo, West Pokot, Nakuru  na maeneo mengine .