JUJA: Mgombeaji Francis Waititu Apige Kura Huku Akiwa Amepiga Magoti (PICHA)

Siku ya Jumanne wakenya wa tabaka mbali mbali kote nchini walijitokeza kwa wingi ili wapigie wagombea wanaowapenda kura, huku wakivumilia baridi kali na mistari mirefu.

Katika shughuli hiyo ya upigaji kura, visa kadhaa vimeripotiwa katika vituo vya kupigia kura huku wanawake na wanaume wakitumis kila mbinu ili wapate fursa ya kipekee ya kupiga kura bila kupiga foleni.

Miongoni mwa visa vilivyo ripotiwa ni wanawake kupeana watoto pindi tu wanapopiga kura huku pia wanaume wakiwabeba watoto ili wajaribu bahati yao.

Huku matukio kadhaa yakizidi kuripotiwa, mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Juja, Francis Waititu aliwashangaza wengi alipopiga kura yake huku akiwa amepiga magoti.

Nia yake ya kupiga magoti bado haijulikani lakini amewawacha wengi vinywa wazi. Tazama picha ifuatayo.