Juju! Ndoa yangu ilikatika ghafla baada ya kuitumia vibaya ‘dawa ya mapenzi’

  Kuna nyimbo nyingi sana  zimeimbwa kuhusu mapenzi lakini wimbo mmoja ambao unajirudia katika akili zangu ninapojitayarisha kwa  mahoajino na  Anita  Baraka  kuhusu masaibu ya ndoa yake na jinsi alivyofanya anachojutia ili kupendwa ni  wimbo wa Ali Kiba – Mapenzi yanarun dunia.

Kila  mtu anatamani sana kumpata mwenziye anayempenda sana lakini kuna wanaoamua kutumia njia ya mkato ili kupendwa na wengi hasa huwa ni akina dada . Mwanamke ukimwambia kwamba kuna njia ya kumsaidia amfanye mwanamme mmoja ampende kabisa basi atafanya kila utakachomuambia na ndio masaibu ambayo Anita alijkuta .  Miaka mine iliyopita akiishi Bombolulu amesikia kuhusu mwanamke katika eneo hilo ambaye alilkuwa kamwendea kwa werevu mume wake akampenda kupindukia na pia akawa kama kijibwa.Mke alipokuwa akisema lolote basi mume wake lazima angefuata masharti  na kuitikia kila takwa la mke wake .Anita alitamani sana kuwa na maamlaka kama hayo kwa mwanamme na hata iwapo italazimu kutumia nguvu za ‘werevu’ au ukutaka tuseme bayan basi mganga .

Ikawa sasa anatafuta njia ya kutambulishwa kwa mwanamke Yule ili amsaidie naye pia apate dawa maalum ya kuweza kumanasa  na kumweka chini ya nguvu  za dawa ya kiasili mume wake .Alitaka apendwe kuliko chochote! Akafaulu kutambulishwa kwa Yule mama baada ya kufanya urafiki naye kwa muda basi akamwambia alichotaka . siku ya siku ilipofika waliifunga safarai kwenda nchi Jirani ya Tanzania –ikidaiwa huko ndiko mtaalam wa mambo hayo alikuwa . sehemu hasa waliokwend inaitwa Litimbo mpaka wa Tanzania na msumbuji huko chini . Basi ikawa walipokuwa safarini  Anita aliulizwa na Yule ya rafiki yake alitaka dawa gani  hasa kuna aina nyingi za dawa ya mapenzi . Aliambiwa kuna  ya kumfanya mume  awe kondoo au zuzu, ya kumfumba macho mumewe aweze tu kumpenda yeye, Ya kumfanya aisweze kuwa na hamu na mwanamke mwngine nje ya ndoa , ya  kumkanganya asiweze kuamini chochote kischotoka katika kinywa cha mkewe na  hata dawa ya  kupoza uume wa mumewe endapo atajaribu kushiriki tendo la ndoa na mwanamke mwingine !

Hapo ndipo sakata ilipoanza .Anita alishangaa ni ipi kati ya zile dawa alizozitaka na ikawa mtihani mkubwa kwake ,gari linapoelkea  kwa mganga alifaa kuwa na jibu ndiposa wanapofika tu hivi aseme dawa aliyotaka wapewe kasha waanze safari ya kurejea Kenya . Anita alitumia muda ule kufikiria kuhusu ujeuri wa mume wake na jinsi siku hizi hampendi kama ilivyokuwa zamani .Alikuwa na hamaki kuhusu jinsi mumewe alivyojaa na nambari za wanawake wengine katika simu  yake ya mkononi na akajutia mbona  amekuwa mpole sana ili kumruhusu kuendelea kumfanyia dharua baada ya ndoa yao  ya miaka tisa . Akakata kauli kwamba atazitaka dawa zote zile!

  ‘NATAKA ANIPENDE ZAIDI ,AWE KAMA ZUZU NA PIA ASIWAHI KULALA NA MWANAMKE MWINGINE ILA MIMI ‘ Anita alimuambia rafiki yake .

Walijiuliza iwapo kweli dawa hizo zitatolewa kwa pamoja lakini wakasema watafika kwanza kwa  Yule mwerevu wao ambaye atawaambia walichofaa kufanya . Walipofika  Litimbo, walilala kwanza kwa mzee Yule kwa sabahu ya chovu wa safari ndefu na keshye asubuhi wakakubaliana kwamba mzee atawahudumia .ilipofika asubuhi basi Anita akaitwa na mganga ili aseme  kilichompleka Tanzania . Basi akasema mahitaji yake yote na hivyo Mzee mtaalam wakaachwa jukumu la kutafuta dozi tosha . Baada ya kumuangalia Anita akaona kweli huyo ameshakata uamuzi wa kuitaka dawa hii ,mzee alimpa masharti  na ilani pia .

‘ Dawa hii imechanganywa ili kutekeleza vyote unavyotaka.Lakini itumie kama nitakavyokueleza.Ukikosea hivi basi utavuruga kila azimio lako na hata huenda huyu mume asiwe wako tena’

 

Maneno hayo  yalimtisha Anita lakini fikra ya kuweza kupendwa kupindukia na mumewe haingemruhusu kujiingiza woga wakati ule na basi akakubali na dawa iliyochanganywa ambayo hakuna anayejua vimesagwa nini  vikakorogwa pale akapewa mtoto Yule wa kike .Tayari kurejea Kenya kwa mumewe ili sasa amteke kwa mapenzi bandia –Mapenzi ya mti…… yaani mapenzi ya dawa . Njia za mkato zina mambo! Ilivyofaa kutumiwa ile dawa ni kwamba Anita alifaa kuiweka kwenye kikeombe chai ya mumewe kisha akinywa hivi basi – dume litazidisha dozi ya love.

‘Akasema pia nilifaa kuinyunyiza nyingine katika kitanda chetu alafu  ya mwisho nilifaa kujipaka katika  sehemu zangu za uke '

Alivyoelezwa  Anita ,ililikuwa sasa kibarua ni kwake kufanya alivyoambiwa nay eye na rafiki yake wakafunfa sagari ya kurejea .Ila unachopanga wewe ,kuna mkuu aliyepanga mbele yako na kwa bahati mabaya au nzuri – Anita hakuelewa ama hakujua kwamna dawa hii ni yeye aliyefaa kuitumia .Alipofika Bombolulu , Mombasa ,kwa sababu ya shughuli zake na kwa ajili pia huwa hampikii mumewe kwa sababu kuna  mfanyikazi wa nyumbani ,Anita alimpa maelekezo Yule mfanyikazi wa nyumbani .Kwamba akishapika chai basi katika kikombe cha mumewe amuekee hiyo dawa  akisema ni  kiungo tu cha chai .Msichana wa kwazi akaelewa masharti ya mwajiri wake na akatekeleza vile . Pia  Anita akienda kazini akuamchua msichana wa kazi shughuli ya pili kwamba akitayarisha chumba chao cha kulala ,basi hii dawa nyingine iliyokuwa na mvuto mzuri aimwagulie pale kitandani  alafu aendelee na shughuli zake .

Duh! Kufikia sasa unajua kilichofanyika .Mumewe Anita badala ya kumpenda mke wake alimpenda mfanyikazi Yule yaya wa nyumba ambaye ndiye aliyekuwa akimpa ile dawa katika chai na hata kuitia katika kitanda chake . Ikawa kwa siku chache tu yule yaya akashangaa kimefanyika nini kwa sababu baba mwenye nyumba sasa alianza kumsifia kuhusu urembo wake na bidii aliokuwa nayo. Kidogo akaanza kumpigia simu akiwa kazini  kumjulia hali .Muda mfupi baadaye maskini mumewe Anita alijikuta ametoroka kazini amerejea nyumbani ili kula tamu na mfanyikazi wa nyumbani wakati Anita yupo kazini . Ugunduzi wa Anita kuhusu makosa aliofanya ulimjia too late na kufikia wakati huo ,mumewe hakumsikiza yeyote isipokuwa yule mfanyikazi wa nyumbani ambaye sasa ilikuwa wazi kwamba walikuwa wapenzi .Hivyo ndivyo dawa ya mapenzi ilivyoikatiza ndoa ya Anita kwa ghafla.

‘Haya mnayoyaona katika  filamu za Nigeria hayafanyiki tu afrika magharibi,mambo haya yapo hapa pia’ Anita anatamatisha.