juliani.1

Juliani apasua mbarika, afichua wakati walitengana na Brenda Wairimu

Kwa mda sasa, wengi wamekuwa wakingoja msanii mashuhuri, Julius Owino almaarufu, ‘Juliani’ apasue mbarika kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mpenziwe, Brenda Wairimu ambaye ni mwigizaji.

Juliani na Brenda Wairimu wamejaliwa mtoto mmoja wa kike mwenye urembo kupindukia.

Mapenzi ya wawili hawa yalipendeza wengi huku wengi wakiotea penzi lao na kusifia jinsi wawili hao walikuwa wakiendeleza uhusiano wao, haswa huku kila mtu akiwamulika.

Hata hivyo, kumekuwa na tetesi kuwa wawili hao wametengana kwani hata hamna aliyekuwa akichapisha picha za mwenzake katika mitandao ya kijamii wala kuzungumzia uhusiano wao.

Hata hivyo, msanii huyo wa ‘Bahasha ya Ocampo’ amepasua mbarika kuhusu uhusiano wao katika mahojiano ya moja kwa moja na mwanahabari, Betty Kyallo katika kitengo chake cha Up Close.

Juliani aliwashangaza wengi alipofichua kuwa umekuwa mda wa miaka miwili tangu watengane na Brenda.

 

Hatujakuwa pamoja kwa miaka miwili. Brenda ni mzazi mwema na binadamu wa maajabu. Amekuwa akinisaidia kumlea mwana wetu wa kike.

Kama binadamu yeye ni wa maajabu sana na namwombea kila la heri. Juliani alisema.

Betty kwa upande wake alipenda kujua jinsi uhusiano wake na mwanawe upo na msanii huyo alikiri kuwa Brenda humruhusu awe na uhusiano na pia kuwa na mda na mwanawe.

Nilikaa naye kwa mda wa siku nne juma lililopita na mamake huniruhusu kuwa katika maisha ya mwanangu na mimi hujaribu kila niwezalo kuwa baba mwema. Naweza mchukua kila nitakapo.

Kitengo hicho ambacho mara nyingi wanaofanyiwa mahojiano huwa mitaa au nyumbani mwao lakini hili halikufanyika na Juliani. Je mbona?

Hatukuanzia nyumbani kwa sababu nilihitaji kuwa mahali hamna anayejua. Mahali naweza fanya chochote bila yeyote kunihukumu.

Lakini ni kipi alichojifunza kutoka kwa uhusiano wake?

Hata mtu akifanya makosa unahitaji kumuelewa kwani ni binadamu na ushughulike na kitu kimoja na uweze kusaidi kutoa uzuri kutoka mtu yule. Sio kila wakati mambo ya kupokea bali pia kupeana.

Sihitaji mapenzi sasa, nina upendo wa kutosha kwa Dandora.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments