Jumba la poromoka Kericho, watu kadhaa wahofiwa kukwama ndani ya vifusi

Watu kadhaa wanahofiwa kukwama katika vifusi vya Jumba la ghorofa 4  mjini Kericho baada ya Jumba hilo kuporomoka.

Habari za awali zaonyesha kuwa huenda takriban watu 70 walikuwa ndani ya jumba hilo lililoporomoka mwendo wa saa mbili usiku siku ya Jumanne.

Mafisa wa uokoaji wamekuwa wakiendelea na juhudi za kuokoa wahasiriwa huku maafisa wa polisi wakishika doria.

Inasemekana Jumba hilo kwa jina 'Tebsview' linamilikiwa na mfanyibiashara mmoja mjini humo huku ripoti za awali zikidokeza kuwa huenda ujenzi mbovu ulichangia kuporomoka kwa jengo hilo.

Waliokuwa karibu wanasema kwamba watu kadhaa walikuwa wakisikika kutoka ndani ya vifusi vya jengo hilo wakiomba kuokolewa.