(+ JUMBE) Rayvanny atemwa na mkewe, jumbe zavujishwa Insta

Staa wa ngoma ya Tetema kwa sasa anazongwa fikra baada ya kutemwa na mkewe Fahy Vanny.

Kwa mujibu wa posti aliyoichapisha Insta, jumbe za mkewe za kutotaka tena mahusiano ni ishara tosha kuwa ndoa yao imeingia shubiri.

Fahy Vanny anasema kuwa maisha ya ndoa na RayVanny yamemfika mwisho.

https://www.instagram.com/p/B5NYgU2A9jn/

Katika ujumbe uliojaa machungu,mkewe anampa msomo Rayvanny kumkoma na kumsahau mtoto wao Jaydan.

“Hesabu mimi na Jay amefariki kwenye maisha yako. Nitapigana na nitashinda. Sitakosa pesa ya kula. Ila mimi na Jay hesabu kuwa tumekufa kwenye maisha yako," aliandika Fahy katika mtandao wa Insta.

Rayvanny alimjibu kuwa mkewe amekuwa akitamani maisha yasiyo na tija yoyote.

Huku akionyesha ishara ya kukubali matokeo, staa huyu alimtakia mkewe mema na kudokeza kuwa bado anaipenda familia yae.

“Nimekuwa Nakuheshimu miaka tuliokuwa pamoja. Kuna mengi tumekoseana na tumesameheana na kila mara umekuwa ukitamani maisha ambayo kila siku nakwambia hayatakusaidia,"

"Nakuheshimu na naiheshimu sana familia yangu. Ikiwa umeamua mwenyewe kuondoka, siwezi kulaumu. Bado napenda familia yangu. Nakutakia Maisha Mema,” aliandika Rayvanny.