Junet atishia kumshtaki Khalwale kwa matamshi kuhusu pesa za Covid 19

Khalwale
Khalwale
Mbunge Suna mashariki Junet Mohamed ametshia kumshataki seneta wa zamani  wa kakamega  Boni Khalwale   kwa kudai kwamba amelipwa pesa za kupambana na janga la Covid 19

Kupitia mawakili wake Junet amesema matamshi hayo ya Khalwale  yamemsababishia  fedheha na usumbufu  na kumpa hofu kando na kumsababishia mawazo .

Junet  amesema  Khalwale,  alipokuwa Busia kwa mkutano wa hadhara mapema mwezi huu alidai kwamba  Junet amelipwa pesa za shirika la Kemsa  ambazo zilifaa kutumiwa kupambana na janga la corona nchini

Khalwale aliongeza kwamba mwakilishi wa akina mama wa Homabay Gladys Wanga aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya fedha ili kufanikisha malipo hayo .

Kulingana na mawakili hao , Khalwale alimtaka rais Uhuru Kenyatta kumfuta kazi wazii wa Afya Mutahi Kagwe kwa kuruhusu pesa za Covid 19 kulipwa kwa  katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju na Junet

Mawakili hao wamesema  iwapo khalwale hatoomba msamaha na kutekeleza masharti yao katika siku tatu zijazo wataanzisha utaratibu wa kumfikisha kortini .