Junior Nyong'o amuoa mpenziye msanii Wanja Wahoro

Mwanawe gavana wa Kisumu Anyang' Nyongo Junior Nyong'o amefunga pingu za maisha na mpenzi wake Wahoro Wanja kwenye harusi ya kufana na kupigwa mfano na wengi.

Msanii huyo ambaye anaishi Marekani alimuoa Wanja Wahoro baada ya kuchumbiana na kwa muda.

" Nitatembea na wewe milele, katika safari ndefu yenye mabonde na milima, nitakupenda kwa roho yangu yote na kila mtu atashuhudia upendo wangu kwako.' Junior Nyong'o Alizungumza.

Kwa upande huu mwingine Wanja naye alikuwa na haya ya kumwambia mpenzi wake;

“You are a fixed point in my universe, and the best friend I’ve ever known. ‘🧡

Not the wedding we planned originally, but ultimately even more perfect and intimate than we could have ever imagined. So many thanks to @zereniti_house for hosting us SO wonderfully.”

Msanii huyo ambaye anatambulika kwa ubunifu wa aina kadha wa kadha wa kimavazi, aliwahi kashifiwa kwa wakati mmoja kwa kuwa shoga.

Dada yake lupita Nyong'o ambaye hakuweza kuhudhiria harusi yao aliwatumia ujumbe wa kuwapongeza.