Kabarak yaongoza katika mtihani wa KCSE

Picha: mediamaxnetwork.co.ke

Kabarak High School ndio shule iliyosajili matokeo bora zaidi katika mtihani wa KCSE wa mwaka jana kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kupata jumla ya alama 11.667.

Kati ya watahiniwa 289 katika shule hiyo, 202 walipata gredi ya A huku mtahiniwa aliyepata gredi ya chini akipata B. Hatua hiyo inaamisha kwamba darasa hilo zima linafuzu kujiunga na chuo kikuu.

Katika nafasi ya pili ni Maseno School iliyopata jumla ya alama 11.393. Kati ya watahiniwa 285 ,140 walipata gredi ya A ilhali 122 wana gredi ya A- . shule ya Wavulana ya Alliance inafunga tatu bora kwa jumla ya alama 11.37. Shule ya wavulana ya Chavakali hata hivyo ndio iliyovunja rekodi kwani watahiniwa wake 300 walipata gredi ya A.