Masanduku amesema kuwa penzi hilo lilimwadhiri hadi kwenye taaluma yake ya Muziki.
"Hii ndio sababu niliacha kufanya tasnia ya ucheshi kwani nilikosa sababu ya kuwafurahisha wengine ilihali mimi mwenyewe sina furaha." Masanduku alisema.
"Tulipeana talaka kwa amani tu na mimi namshukuru mungu kwa kuwa alikuwa na utu uzima kwenye wakati huo wote. Hata hivyo, Talaka ni jambo mbaya sana."
JB Masanduku amewapa ujumbe wazazi wanao wanyima waenzao nafasi ya kuwaona wanao." Mtoto atazidi kukua na akifikisha umri wa miaka 18 atakuwa na dai la kutaka kumwona babaye na hivyo atajua tu kuwa ni mamaye alimyima hio nafasi na hilo jambo sio jambo nzuri."
Pamoja na hayo, Masandukuhakutaja sababu inayomfanya Kagia kumyima nafasi ya kuwaona wanawe wawili.