Kakake Nicki Minaj ahukumiwa miaka 25 jela kwa kumbaka binti yake wa kambo.

Kakake msanii wa Marekani Nicki Minaj Jelani Maraj,  atasalia jela kwa miaka 25  baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake wa kambo  mwenye umri wa miaka 11 .Jaji amesema Maraj ‘ameharibu’ mtoto huyo .  Jaji  Robert McDonald  amesema Maraja anastahili adhabu hiyo ua miaka 25 jela kwa sababu alimbaka mtoto huyo mara kwa mara .

“ ULIMBAKA HUYU MTOTO .ULIMBAKA MARA  KWA MARA’ amesema jaji  Mcdonald

Kakake mwathiriwa alishuhudia Maraj  alimdhulumu dadake na kawaambia maafisa wa shule yake .Nicki Minaj  hakuwa kortini siku ya jumatatu ili kuwa na kakake mkubwa .Maraj  aliiomba mahaama kumpa msamaha akisema kwamba hakuekeleza kitendo hicho .

“ NINGEPENDA KUOMBA RADHI KWA  MACHUNGU NILIYOSABABISHA .NILIKUWA  NA TATIZO LA KUNYWA POMBE  KUPINDUKIA  NA NAOMBA MSAMAHA KUTOKA KWA KORT’ Alisema Maraj .

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa  mwathiriwa  ambaye ni binti yake wa kambo aliambia mahakama kwamba dhulma hizo zilimfanya kutaka kujiua .

“ SIKUFIKIRI NINGEMALIZA SIU KABLA YA KUPATWA NA KISA CHA KUTAKA KUJIANGAMIZA .NILIHISI KWAMBA SIKUWA NA SAUTI’

Jelani Maraj   ameshtumiwa kwa kumbaka mara kadhaa  binti  yake wa kambo  katika boma la familia ya  Baldwin. Maraj alikanusha madai hayo akisema  madai hayo ni wongo yaliyolenga kumpunja dadake Minaj,pesa .