Kakamega: G3 Recovered

Polisi katika kaunti ya kakamega wamewakamata washukiwa wawili na kupata bunduki moja aina ya G3 inayosemekana kuwa moja ya zile zilizoibwa katika kituo cha polisi cha booker mjini mumias

Kamanda wa polisi eneo la magharibi moses ombati amesema washukiwa hao walikuwa miongoni mwa genge lililokuwa likijaribu kutekeleza uhalifu eneo la mayoni.