Kama Bosi![Picha] Waiguru aonekana akicheza 'solitaire' wakati wa kikao cha kumfurusha afisini

Gavana  aliye mashakani wa Kirinyaga Anne Waiguru  siku ya Jumanne amepigwa picha akiwa katika simu yake Solitaire wakati kesi yake ya kufurushwa afisini ilipokuwa ikisikizwa na senate .

Solitaire ni mchezo wa kadi katika simu ambao  pia unaweza kuchezwa  katika kompyuta ili kupitisha muda .

Mchezo wa  classic Solitaire  mwanzoni huonekana kuwa kibarua lakini baada uzoefu mtu huweza kujitambua kiubabe .

Katika picha zilichokuliwa na gazeti la The Star  Waiguru alionekana akijishughulisha kwa umakini na mchezo huo katika simu yake na kusaliti  muonekano wa mambo yake kuwa magumu baada ya waakilishi wa kaunti kupiga kura ya kumtoa afisini na kufikisha lalama zao mbele ya senate .

Akizungumza  mbele ya kamati inayosikiza madai dhidi yake Waiguru amesema madai yaliyotolewa na wakilishi hao hayana msingi na yametegemea hila dhidi yake kwa lengo la kumhujumu na kumfedhehesha .