'Kama hatakuoa rudi nyumbani,' Baba yake Akothee amwambia Cebie

Dada yake msanii Akothee, Cebie amepanga kufunga pingu zake za maisha mapema mwaka ujao, huku akiolewa na mpenzi wake Juspus Rusana aliyemposea Julai mwaka huu.

Baada ya hafla hiyo Cebie alizungumza kuhusu harusi yake na kwanini haswa hajaweka hafa hiyo mwaka huu;

"Virusi vya corona vikiisha ndio nitafunga pingu za maisha mapema mwaka ujao, kwa maana familia yetu ni kubwa serikali haiwezi kubali wote kuhudhuria harusi yangu, wajukuu 64 na ndugu 24 hao ni watu wengi." Alisema Cebie.

Pia alifichua kuwa baba yake alisikia kesi yake ya ukafiri baada ya kufichuliwa na Edgar Obare na hisia zake ziligusa moyo wake wote.

"Alinipiga simu na kuniambia napaswa kuwa nguvu kwa maana hayo ndio maisha, aliniambia hata huyu hasiponioa nirudi nyumbani hamna shida

Aliniambia mimi ni mali nisiwache mtu anisaliti, mama yangu alikuwa maekasirika sana kwa maana ni mwalimu na pia mwanasiasa." Alisema.