"Kama hatufanyi Twa Twa Twa na wewe, koma kufuata hali yangu ya UKIMWI," afoka Akothee

26F76347-EA10-4748-A987-F1257B8E1D82
26F76347-EA10-4748-A987-F1257B8E1D82
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Akothee amewapiga kijembe wanaochunguza kujua hali yake kuhusu kama ana virusi vya UKIMWi au la.

Katika mtandao wa Insta, Akothee ambaye anahisi vizuri baada ya kupata afueni ya haraka amefunguka haya.

"...Tafadhali kama hatushiriki Twa twa twa pamoja, ina umuhimu gani ujue hali yangu ya kiafya kuhusu UKIMWI? KOMA" Aliandika katika mtandao.

Haya yanajiri siku chache baada ya mama huyu wa watoto watano kuanguka na kuzirai stejini akitumbuiza.

https://www.instagram.com/p/B55VzT2n_xf/

Tukio hili liliwashangaza mashabiki wake na wakatuma pole na jumbe za kumtakia afueni ya haraka.

Meneja wake alisema kuwa staa huyu alishikwa na kizunguzungu kufuatia uchovu mwingi.

Akothee ni msanii na ambaye hufanya majanga makubwa stejini.

Tukio la Akothee kuanguka ghafla na kuzirai akiwa stejini liliwafanya wengi kuzungumza sana katika mitandao ya kijamii.

Tukio hilo liliwashtua watoto wake huku binti zake wakimtumia jumbe za kumtakia afya njema.

Wengi wa mashabiki walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa burudani wikendi katika fiesta waliposhuhudia kisa hiki.

Akothee kupitia mtandao huu pia ametangaza kuwa amepanga safari ya kuwapa chakula cha msaada wakaazi wa kutoka maeneo ya Turkana.