Kama hatuna mahusiano ya kimapenzi usiseme tuna mahusiano,' Diamond awaonya wanadada wanaosema wana mahusiano naye

Diamond
Diamond
Bosi wa lebo ya WCB na staa wa bongo Diamond Platnumz amejitokeza na kuwaonya wanadada ambao wanadai kuwa wana uhusiano wa kimapenzi naye.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii, Diamond alisema kuwa anawapenda wanawake kwa maana huwa wanamuunga mkono katika usanii wake. Lakini si vyema mtu kujitokeza na kusema kuwa nina mahusiano ya kimapenzi naye.

Chibu aliwapa onyo kali kwa wanadada wanaosema madai hayo na kusema kuwa hivyo ni kumharibia jina hasa katika sekta ya usanii.

Pia alisema kuwa si vyema kwake kuanza kuwaaibisha watu hadharani kwa jambo ambalo wanaweza kutatua na kuachana nalo.

“Nashukuru sana kwa upendo mkubwa wa madada mbalimbali ambao unazidi kuongezeka siku hadi siku juu yangu…nawathamini na nawapenda Zaidi… ila tafadhali, kama unajua hatujawahi na wala hatuna mahusiano ya kimapenzi, usiseme tuna mahusiano maana inakua haikai vyema… na pia kibinaadamu si sawa kwa mimi sasa hivi nianze kumtoa mtu nishai mtandaoni… nawapenda sana na nawashukuru kwa support kubwa mnayonipa #WCB4LIFE." Diamond Aliandika.

Hili linajiri siku chache baada ya mwanamke anyefahamika kama Husna Maulid  kuposti picha za Chibu zikiwa na jumbe tofauti na kuwaacha wengi wakizungumza.

Hii si mara ya kwanza mwanamke kudai kuwa ana uhusiano na Chibu na kuwa ana mtoto wake. Ripoti pia zilidai kuwa Diamond amemkondishia mwanamke huyo nyumba.