Kama hujaoa ,Warembo ndio hawa,fursa ndio hii

Iwapo una ‘roho’ kama wanavyosema wakenya  kumaanisha ujasiri na huna mke, basi pata kujua kwamba una fursa ya wazi  hapa endapo utafaulu  kumshawishi mmojawapo wa mabinti hawa wa nasiasa wa humu nchini kufunga pingu za maisha nawe .

Wanasiasa wa humu nchini wanapokea donge nono na bila shaka binti zao pia wanaishi vizuri, nani hataki kupata mke ambaye  ana kipato kizuri?

Kwa walio na ukakamavu basi orodha  ndio hii hapa;

1.Ngina Kenyatta

Binti huyu wa rais Uhuru Kenyatta na ama Marget Kenyatta  alioekana mbele ya umma kwa mara ya kwanza mwaka wa 2013  wakati babake alipokuwa rais. Wakati ambapo ameonekana katika hafla za umma, tumeona wanaume wakimmezea mate akiwemo Eric Omondi .

  1. Andrea Kenneth

Binti yake Peter Kenneth  alisababisha mtikisiko wa mtandaoni alipotambulishwa kwa umma pamoja na kakake Andrew Kenneth wakati wa uzinduzi wa kampeni ya  kuwania urais ya babake mwaka wa 2013. Andrew pia aliwavutia wengi kwa kutoa himizo kwa wapiga kura kumchagua babake kuwa rais .

  1.  Lupita Nyong’o

Mshindi huyo wa tuzo ya Oscar  ni binti yake gavana wa Kisumu Anyang’a nyong’o. Lupita ni muigizaji wa filamu na ameipa Kenya  sifa hasa baada ya hotuba yake  iliyopewa wakenya kwamba kila mtu anaweza kutimiza ndoto yake maishani. Anazungumza  kihispania, Kiingereza, Luo na Kiswahili .

  1. Tallisa Moi

Ni mjukuu wa  rais wa pili wa taifa  Daniel Arap Moi  na binti yake Philip Moi. Ametambulika sana kwa kupenda kutumia mitandao ya kijamii na wakati mmoja ulizagaa uvumi kwamba yupo katika uhusiano na mwanawe rais Uhuru Kenyatta .

  1. Makenna Maria Ngugi

Ni binti yake mwakilishi wa kina mama wa Nairobi Esther Passaris. Makena pia ni msani na mara ya kwanza alitambulika akiwa na umri wa miaka 16  alipoonyesha ustadi wake wa kufoka mistari.  Kazi ndio hiyo sasa.