Lazima ningemwita Raila ‘Baba’- Moses Kuria asimulia masaibu yake Mombasa

kuria
kuria
 

Mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria  amesimulia yaliyomfika siku ya  jumamosi wakati wa mkutano wa BBI katika bustani ya Mama Ngina waterfront . Kuria amesema ilikuwa lazima kwa kila aliyezungumza kumwita  Kiongozi wa ODM ‘baba’ ili kuwa na amani ." ilikuwa ni kama hitaji la kikatiba kumwita Raila ‘Baba’   Kuria amesema .Amesema kiti chake na kofia vilitwaliwa kwa muda kwa sababu alikataa kusimama wakati Raila alipoingia jukwani .

Amedai kwamba kuna baadhi ya viongozi wanaoitumia ripoti ya BBI kuanzisha kampeini za mwaka wa 2022  na kamwe hatokuwa miongoni mwa watakaolazimishwa kumuunga mkono Odinga kuwa rais ." Kama kumuunga Raila mkono kuwa rais ndio tiketi ya kwenda binguni ,basi heri niende jehanamu’ amesema Kuria . Ameongeza kwamba anaiunga mkono ripoti ya BBI na sio  kiongozi wa Odm Raila ." Ndio kwa BBI ,Hapana kwa Raila’ ameongeza Kuria .

Huko Mombasa siku ya jumamosi Kuria alikuwa miongoni mwa viongozi wa kundi la tanga tanga waliovurusgwa na  walinzi katika jukwaa kuu la mkutano lakini wakazuia jaribio la kuwazuia kuingia katika jukwa hilo . Mbunge wa Nyali  Mohammed Ali pia alilazimika ‘kukipigania’ kiti chake akisema kwamba alichaguliwa na hivyo basi alikuwa na haki ya kuketi jukwaani . Alimshtumu mbunge wa Suna mashariki Junet Mohammed kwa kumwonea na kumlenga  kabla  kuurusha mkono wa Junet.  Gavana wa Mombasa Hassan  Joho na mbunge wa Mvita  Abdulswamad Nassir  walilazimika kuingilia kati ili kurejesha utulivu . Kipchumba Murkomen ndiye kiongozi pekee wa Tanga tanga aliyeruhisiwa kuutubia mkutano huo .