'Kama nachinja ngombe who are you?' Mwanamke aeleza masaibu mikononi mwa mumewe

Radio Jambo's Massawe Japanni
Radio Jambo's Massawe Japanni
Mwanadada kwa jina Purity aliwashangaza wengi alipopiga simu katika kipindi cha Bustani la Massawe cha mtangazaji, Massawe Japanni kuelezea masaibu aliyokumbana nayo mikononi mwa mumewe.

Purity alikuwa anachangia katika mjadala ambao uliwaleta wana ndoa pamoja na kuwapa fursa ya kuelezea waliyopitia kati ndoa zao, na jinsi walivyo tatua yote.

Aliwashangaza waskizaji na pia Massawe Japanni alipofichua kuwa mumewe amekuwa akimtishia mara kwa mara kuwa anaweza mchinja.

Isitoshe, mumewe Purity alikuwa anajigamba kuwa ana uhodari wa kuchinja wanyama ikiwemo ng'ombe na basi itakuwa kazi rahisi sana kumchinja mkewe iwapo hangebadilisha mienendo yake.

Hata hivyo, cha muhimu ni kuwa bi Purity aliweza kujinasua kutokana na mtego huo pamoja na mwanawe wa miezi tisa, baada ya kumfungua mumewe kwa nyumba.

Tangia siku hiyo hajawahi tamani kumuona wala kuzungumza na aliyekuwa mumewe hadi wa leo.

Soma usimulizi wake.

"Ah Massawe mimi ndio nilipitia na kwambia, mimi mpaka kisu kunishikia tunang'ang'ana kwa nyumba. Mwishowe nilimfungia kwa nyumba natoroka, alikuwa ananiambia mimi ni kitu kidogo mbele yake kwani yeye hukata ng'ombe.

Mimi unajua nilitoka kwake mara moja hata sijawahi tamani, nilitoka na mtoto wa miezi tisa. Tulipatana naye Eldoret na alikuwa anafanya kazi ya butchery." Alisimulia bi Purity.

Skiza kanda ifuatayo ili upate uhondo kamili.

&feature=youtu.be