Rashid Yakub amehamishwa hadi Nairobu kuwa mkuu wa polisi kutoka kwa Philip Ndolo.
Mabadiliko hayo yameangazwa siku ya jumamosi na Ndolo ataelekea Nyeri kuwa naibu kamanda wa chuo cha mafunzo ya polisi Kiganjo .
Yakub alikuwa kamanda wa polisi wa pwani na disemba mwaka jana alimshtumu gavana wa Nairobi Mike Sonko kwa kumshambulia wakati Sonko alipokuwa akikamatwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Voi kuhusiana na kesi ya utoaji zabuni ya shilingi Milioni 357 .
Baadaye Yakub aliamua kuondoa kesi hiyo dhidi ya Sonko