KAMENUKA: Lazimisheni mashahidi kushuhudia katika kesi ya Moses Kuria - DPP

Mp Moses Kuria
Mp Moses Kuria
Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma imeweza kuamrisha mahakama iweze kulazimisha mashahidi kushuhudia kesi inayo mkumba mbunge wa Gatundu Moses Kuria.

Hii ni baada ya DDP kuwafanyia uchunguzi maafisa ambao walikuwa wanaadai kuwa mashahidi hao hawakuwa itayari kushuhudia kesi hiyo ya matamshi ya chuki.

"mashahidi hao waliweza kundika barua huku wakisema kua hawakua tayari kushuhudia katika kesi hiyo,

"Bali ushahidi wa ni wa maana sana katika kesi hii,tunaomba mahakama iweze kuwaliazimisha waje kutoa ushahidi wao," Mashtaka iliandika.

Manamo tarehe ,9, desember  mkurugenzi wa mashtaka ya kigaidi a umma aliweza kuelekezwa aweze kutambua aliye tatiza ushahidi wa mashahidi hao ifikapo katikati ya mwezi wa januari 2020.

Mahakama ilisikia kuwa ushahidi uliweza kupatikana katika ofisi za mshikamano wa kitaifa na tume ya ujumuishaji.

Hii ni baada ya makosa ambayo yalitokea,walisema kuwa palikuwa na haja ya kuanzisha washahidi wapya ambapo mtetezi aliweza kupinga hoja hiyo.

" Katika hatua hii tunaomba mahakama isikubali mashtaka kuleta washahidi wapya ili kutoa ushahidi wao," Mtetezi Alisema.

Hakimu wa mahakama ya Milimani Kennedy Cheruiyot aliweza kubali mashtaka kuleta mashahidi wapya katika kesi hiyo.

Mnamo novemba 25,2015, mbunge Kuria alishtakiwa katika mahakama ya Nairobi kwa kutamka maneno ambayo yangeleta vurugu na vifo kwa wananchi wa kenya.

Kuria alisema maneno hayo kwa lugha ya mama(Kikuyu).

Inasema Moes Kuria alitamka au kunena maneno hayo alipokuwa katika uwanja wa kaunti ya Kiambu tarehe 26,juni,2015.

Mwaka jana mbunge huyo aliweza kushtakiwa upya kwa madai ya uchochezi ambapo alikataa madai hayo.

Agosti ,2,2019 mahakama iliweza kufutilia mbali kesi hiyi huku wakisema kuwa Kuria hakuwa na kesi yeyote ya kujibu.

Septemba ,5, 2017, mashtaka ilieza kunakili kuwa mbunge huyo alisema maneno hayo  ya matusi akiwa katika soko la wangige na maneno ambayo yangeweza kuumiza mwananchi wa Kenya.

Katika utawala wa hakimu Francis Andanyi a;isema kuwa hakuna ushahidi ulioonyesha Kuria alisema maneno hayo huku akisema kuwa ushahidi huo ulitolewa katika mtandao wa kijamii.

Hiyo ilikuwa mara ya tatu Moses Kuria kukatazwa dhamana kwa kosa sawa.