Kamishna awaonya wakeketeji wa watoto wasichana

Kamishna wa kaunti ya Migori Seif Iddi Matata amewaonya vikali wale wanaoshiriki katika ukeketeji wa watoto wasichana akisema kuwa ni kinyume cha sheria..

Kamishna huyo alisema kuwa dhuluma za watoto wa kike katika eneo la Kuria zimezidi sana na kupelekea watoto wengi kupashwa tohara ambayi ni kinyume cha sheria na kutaka machifu,manaibu wao na pia polisi kushirikiana nao katika vita dhidi ya mila hiyo ambayo imewakandamiza wanawake na wasichana na kulemaza juhudi za ustawi wa watoto wasichana katika eneo hilo.

Kamishna huyo pia aliwaonya wazee wa jamii ya Kuria dhidi ya kuwalazimu wanao wa kike kushiriki katika mila hiyo na kutaka nchi jirani ya Tanzania kushirikiana nao katika vita dhidi ya dhuluma kwa watoto wa kike ambao hupashwa tohara nchini Tanzania na kisha kuregeshwa nchini Kenya baada ya kupashwa tohara na kuozwa kwa watu wenye umri wa juu.