Kampuni bora 100 za kufanyia kazi

safaricom
safaricom
Utafiti uliofanywa hivi maajuzi umebaini kwamba kampuni ya Safaricom yaongoza katika mia bora za kufanyia kazi.

Hii ni mara ya pili mfululizo kampuni hiyo ya mawasiliano kuchukua nafasi hiyo ikizingatiwa kwamba  iliibuka nambari moja mwaka uliopita.

Uchunguzi uliofanywa na wakala Brighter Monday uliotolewa siku ya jumanne, ulionyesha kampuni ya East Africa Breweries Limited (EABL) ipo katika nambari ya pili katika orodha hiyo.

 Katika nafasi ya tatu ni kampuni ya umoja wa mataifa (UN), ikifuatiwa na benki ya KCB ( Kenya Commercial Bank), huku kampuni ya kutoza ushuru nchini (KRA) ikikamilisha  kwenye tano bora.

Kampuni zingine zilizoorodheshwa ni pamoja na Kenya Pipeline, Kengen, PWC, Cocacola, na Kenya airways.

Mkurugenzi mtendaji wa Brighter Monday Emmanuel Mutuma alisema kuwa sifa za ndani za kiwango cha juu kabisa ambacho huzingatiwa zaidi katika kampuni ni ushindani wa malipo, usalama wa kazi, ukuaji wa kazi, dhamana ya fedha na faida za ustawi.

Katika uteuzi wa kampuni hizo, uchunguzi uliangalia sifa ambazo zinahusishwa sana na wafanyikazi ambazo ni utamaduni, ukuaji wa kazi, utofauti, ujumuishaji na malipo ya ushindani.