Kanuni za Mavazi: Mavazi 7 usiofaa kuvalia katika harusi

Kualikwa harusini ni jambo  ambalo mara nyingi huwa ni taadhima kubwa  sana . Rafiki na jamaa zako hukutaka ujiunge nao wanaposherehekea  siku muhimu sana  .

Hata hivyo ,kuna kanuni  zinazofuatwa kuhusiana na mavazi yako . Ni muhimu kufahamu unachofaa kuvalia  ukienda harusini  ili kuonyesa heshima  kwa wanandoa na pia kutoonekana kama doa .

Huu hapa mwongozo  wa   mavazi unayofaa kuyaepuka unapoalikwa harusini .

Usivalie chochote cha rangi nyeupe 

Kanuni ya kwanza katika harusi zote ,wanawake hawafai kuvalia vazi lenye rangi nyeupe  kwani itakuwa ni kumkosea heshima Bi Harusi  na itaonekana kama ushindani  kati yako na  Bi harusi . Ni yeye pekee anayefaa kuonekana  bayana na hivyo basi rangi nyeupe ndio huwa chagul  lake .

Wanaume hawafai kuvalia  tuxedo

Bwana Harusi pia anafaa kuonekana wazi  kwani ni siku yake pia  ,hivyo basi ni vyema kwa wageni wa kiume kuvalia suti badala ya tuxedo. Itaonekana ni kana kamba ulikuja kumpa ushindani Bwana harusi

Usionekane umevalia Denim 

Denims are too casual to wear at a wedding even if you are planning to wear a blazer to make it look smart casual,it's not appropriate for a wedding.

Nguo zenye chungi(uwazi)

Sio vazi linalokubalika kwa sababu litafaa tu kwa wakati wa kujiburudisha na rafiki zako wakati wa  usiku .

Nguo za rangi Nyeusi kote

Rangi nyeusi aghalabu huhusishwa na Maazishi . Kwa hivyo kuvalia rangi hii ni hatua inayoweza kuleta simanzi katika sherehe inayofaa kuwa ya vicheko .

Kaptula

wanaume wanaovalia kaptula  kwenda harusi  hukiuka kanuni muhimu sana . Hili linaweza tu kufanyika endapo umepewa ruhusa ya kufanya hivyo na wanaharusi . vazi hili sio rasmi na halifai kwa harusi .

Nguo zenye mikato mirefu 

Harusi ni hafla ya kuonyesha miondoko na hadhi .Jaribu  kuhakikisha kwamba vazi lako linawiana na mandhari ya sherehe .

Hakikisha mtindo wako unabeba na kutisha  ka njia nzuri .