Kanye West atoa msaada wa milioni 200 kwa jamaa za watu waliouliwa na polisi Amerika

kanye-west-87
kanye-west-87
Msanii Kanye West ametoa msaada wa milioni 200 kwa faamilia ya George Floyd, Ahmaud Aebery na Breonna Taylor ambao waliuawa na maafisa wa polis wa Amerika kutokana na ngozi yao nyeusi .

West vile vile ametenga shilingi milioni 529 kama pesa za kumsaidia mwanawe Floyd, Gianna Floyd kusoma katika taasisi za elimu nchini humu.

Msanii huyo pia ametangaza kuwasaidia wafanyabiashara wa ngozi nyuesi kutoka mtaa anaoishi wa Chicago ili kujiendeleza kibiashara.

Akitekeleza miradi hiyo, Kanye West, mkewe Kim Kardashian aliamua kuwalipia huduma za matibabu wote waliokuwa wanaandamana ili kupinga dhulma dhidi ya maafisa wa polisi.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Kim alikashifu mauwaji yanayolenga watu weusi katika taifa la Amerika akisema sharti haki ipatikane kwa kila mwathiriwa.

“For years, with every horrific murder of an innocent black man, woman, or child, I have always tried to find the right words to express my condolences and outrage, but the privilege I am afforded by the color of my skin has often let me feeling like this is not a fight that I can truly take on my own. Not today, not anymore. Like so many of you, I am angry. I am more than angry. I am infuriated and I am disgusted. I am exhausted by the heartbreak I feel seeing mothers, fathers, sisters, brothers, and children suffering because their loved one was murdered or locked away unjustly for being black. “  Aliandika Kim