Kaput! Harmonize  na mkewe  Sarah wablokiana Instagram, Kunani?

Kinatokota kizito huko Bongo. Huenda  wasanii wa TZ wameanza kuiga mfano wa Simba, Diamond  Platinumz wa kuwaacha wapenzi wao ghafla na kutumia kelele zinazofuata kuendeleza umaarufu wao.

Baada ya karibu mwezi mmoja wa patashika kuhusu kutengana kwa Diamond na Tanasha, kimezuka kipya kwamba huenda msaani mwingine TZ Harmonize  ambaye awali alikuwa katika lebo ya  WCB ameachana na mke wake Sarah . Hii ni baada ya wawili hao kukoma kumfuata kila mmoja katika insta  huku wadau wakipiga vijembe kwamba huenda  kila mmoja amemlisha mwenzake bonge la Block .

Ushahidi pia umezuka kuonyesha kweli hakuna kati yao anayemfuata mwenzake katika instagram jambo linalozidisha uhalali wa uwezekano wao wa kuachana .

Harmonize kwa sasa anazidi ku promoti wimbo wake mpya  na hajasema lolote kuhusu uwezekano wa kutengana na Sarah .

Sarah hata hivyo huenda ametoa taswira ya mambo yalivyo kwa ujumbe fiche aliouweka katika insta story yake na kusema ;

“SHE’S IS BROKEN BECAUSE SHE BELIEVED. HE’S OK BECAUSE HE LIED.”