Msanii huyo alieleza mambo mengi yaliyofanyika katika maisha yake baada ya yeye na Diamond kuanza uhusiano . Donna alieleza kwamba mwanzoni mwa uhuisiano huo, mpango wake haukuwa kupata mimba na Staa huyo wa muziki. Alifichua kwamba Chibu alitaka kumuoa baada ya kujuana naye kwa miezi mitatu na alishangaa sana alipogundua kwamba alikuwa mjamzito .
”I was careful not to fall in love with him completely because I wanted to know him better. I was shocked to learn I was pregnant for him. I was not ready to be a mother. It happened because I was not keeping track of my menstruation cycle,” alisema Tanasha
Donna anasema baadaye alianza kufikiria kuhusu kuitoa mimba hiyo. Hata hivyo anasema licha ya kuwaza kuhusu fikra hiyo amefurahi hakuchukua uamuzi huo .
”I really thought of terminating the pregnancy and also promised myself to be more careful next time, should I have gone the termination way, but thank God I did not go through with my thoughts,” Tanasha aliongeza
Kitu kizuri ambacho kiliibuka kutoka kwa uhusiano wake uliofeli na Diamond ni mtoto wao wa kiume aliyezaliwa Oktoba mwaka jana na kuitwa Naseeb Junior.
Kulikuwa na madai kwamba Diamond hakufanya rasmi uhusiano wake na Donna kwa ajili alishauriwa dhidi ya kumuoa mwanamuziki mwenzake kwani pangetokea ushindani .
Diamond amesalia kimya kuhusu kukatika kwa uhusiano wake na Tanasha na itachukua muda kabla ya kufahamu msimamo wake kuhusu kilichotokea .