Kasisi mmoja wa katoliki huko Meru ameuawa kwa kudungwa kisu na mtu asiyejulikana .
Mkuu wa polisi wa imenti kaskazini Robinson Mboloi amesema kasisi huyo aliaga dunia papo hapo kwa kupoteza damu nyingi .
Kiini cha shambulizi hilo hakijajulikana lakini watu wawili waliokuwa wakilewa naye wamekamatwa ili kuwasaidia katika uchunguzi wao .