Kulingana na tathmini ya ripoti za hapo awali, Sudi amedumisha sifa yake hiyo ya kutosema lolote bungeni tangu mwaka wa 2017. Mbunge huyo ni mtetezi mkubwa wa naibu wa rais William Ruto na amekuwa akitoa maoni kuhusu masuala ya kisiasa
Ripoti hiyo imeonyesha kwamba seneta wa Busia Amos Wako hakuzungumza katika seneti mwaka jana pamoja na viongozi wengine walioteuliwa
Viongozi hao ni miongoni mwa wajumbe 25 katika seneti na bunge la taifa ambao wametajwa kwa utendakazi mbovu katika kipindi hicho. Seneta wa Kajiado Philip Mpaayei, wenzake wateule Christine Zawadi na Mercy Chebeni walitajwa kwa utendakazi adimu.
Seneta Ledama Ole Kina (Narok) alitajwa kama mchapakazi zaidi katika seneti.
Alifuatwa na Moses Wetangula (Bungoma), Aaron Cheruiyot (Kericho), Ochilo Ayako (Migori) na Getrude Musuruve (Mteule).
Katika bunge la taifa mbunge wa Mumias Mumias West John Naicca; Samuel Arama (Nakuru West); James Gakuya (Embakasi North); George Aladwa (Makadara); Abdi Shurie (Balambala) ni miongoni mwa waliotajwa kwa utendakazi mbovu katika bunge na mijadala
Miongoni mwa waliotambuliwa kwa uchapakazi mzuri katika bunge ni Millie Odhiambo (Suba North), David Ole Sankok
( Mteule ), Wilberforce Oundo (Funyula) na Robert Pukose (Endebess).