Kati ya watoto wanne tulionao na mume wangu,wawili ni wa babamkwe,Asema Mwanamke

NA NICKSON TOSI

Maisha yamejaa simulizi zilizojaa kinaya na kila uamkapo asubuhi hukosi kupata taarifa ya kuvunja moyo ama kuhuzunisha kamwe.

Ndoa miaka ya zama iliheshimiwa sana na uhusiano baina ya babakwe na wake wa watoto wao ulisalia kuwa wa heshima baina ya pande zote mbili.

Katika  kisa cha kushtua wengi ,mwanamke mmoja amesimulia kuwa kati ya watoto wao wanne ambao wamebarikiwa na mume wake wa miaka ishirini kwa ndoa ,wawili ni wa babamkwe.

Mwanamke huyo alidai kuwa wakati mumewe alikuwa anafanya kazi Sudan Kusini,babamkwe alianza kumchumbia kwa muda kwa sababu mumewe alikuwa anakawia kurudi nyumbani na labda akipewe likizo ya wiki moja hakuwa anamtosheleza vyakutosha ,jambo ambalo lilimpelekea yeye na babamkwe kuanza kuchumbiana na hatimaye kubarikiwa watoto wawili maishani.

Mume wangu anafanya kazi Sudan Kusini ,na unapata yakwamba anachukua muda mwingi ndio apewe likizo,hata akipewa likizo inaweza kuwa wiki moja ambayo kwangu ni finyu ikilinganishwa na muda wa upweke ambao mimi huwa na msubiri.Kutokana na ubweke huo,babamkwe alianza kunichumbia na kutaka tuwe wapenzi,mimi sikuwa na budi bali kukubali manake kibaridi kilikuwa kinanishinda ksweli,niliamua kuwa mpenzi wa pili wa babamkwe.alisimulia mwanamke huyo.

Baada ya kuamua kuwa mpenzi wa babamkwe,mwanamke huyo sasa anasema walibarikiwa watoto wawili ambao anashindwa kuelezea mumewe jinsi alivyowapata manake huenda mumewe akamshuku kuwa labda aliwapata na mwanamume mwingine .

Kwa sasa ,nimeshindwa nitamuelezea namna gani mumewangu ,naona nikama ataanza kunishuku kuwa nilihanya nje ya ndoa na kuanza kulala na wanaume kiholela na kujaaliwa hawa watoto.naogopa kuwa nikimuambia ni watoto wa babake huenda ikaleta shida kwa familia ,nimeshindwa kabisa ,naona nimemsaliti mume wangu ,alielezea Mwanamke huyo.

Mwanamke huyo sasa anasema baada ya babamkwe kumzalisha watoto wawili ,ameanza kumkosea heshima na wakati mwingine anamtukana na kumuita mjinga matamshi ambayo anasema tangu kuolewa kwa familia hiyo hajawahi kumuita hata siku moja.

Ameeleza kuwa wakati mwingine anawafukuza watoto hao wanapokaribia nyumba yake na hata kuwaita mbwa swala ambalo anasema limemfanya kupatwa na ugonjwa wa moyo.

Je  mumeo akiwa anafanya kazi katika mataifa ya kigeni ,unaweza kubali kuwa mpenzi wa babamkwe na hata kujaaliwa watoto naye?