Katibu mkuu wa chama cha ODM afutilia mbali madai ya kubadilishwa kwa viongozi wa chama hicho Homa Bay

NA NICKSON TOSI

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna ametupilia mbali taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa uongozi wa chama hicho umeamua kubadilisha viongozi wake katika kaunti ya Homa Bay.

Sifuna ametaja madai hayo kama ya kupotosha umma na sasa amesema viongozi wote waliochaguliwa kusimamia matawi tofauti nchini wangali.

Kupitia taarifa aliyoituma kwenye mitandao ya kijamii, Sifuna amesema iwapo kiongozi yeyote anataka kujiuzulu kama kiranja wa chama hicho, kuna taratibu ambazo hufuatwa kabla ya kuafikia uamuzi huo.

Wakati uo huo, Sifuna amemkanya mbunge mmoja ambaye hakumtaja jina katika bunge la Kitaifa kwa kueneza taarifa hizo za uongo.

Hii hapa ni taarifa hiyo