Kaunti kupewa shilingi bilioni 1.2 kwa miradi waliopendekeza

Kaunti kumi na mbili zilizoshiriki katika vikao vya mashauriano ya bajeti ya mwaka 2019-20 wana kila sababu ya kutabasamu kwani wabunge wamependekeza wapewe shilingi milioni moja kwa miradi walioitambua.

Kamati ya tathmini za bajeti imependekeza kuwa pesa hizo zigawanywe kwa usawa kati ya kaunti za Bomet, Nyeri, Laikipia, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Kisumu, Kakamega, Wajir, Isiolo, Embu, Taita Taveta, and Lamu.

Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wa ambaye ni mwenyekiti wa kamati hio anasema pendekezo hiloliliafikiwa baada ya mashauriano kuhusu maombi ya matumizi ya fedha kutoka kwa umma.

Matumizi hayo yatanakiliwa katika bajeti iliyopendekezwa ya shilingi trilioni 3.02 ambayo inajumuisha shilingi trilioni 1.9 zilizopendekezwa kutumiwa na idara mbalimbali za serikali.

Waziri wa fedha Henry Rotich Alhamisi hii anatarajiwa kutangaza michakato ambayo serikali itatekeleza, ili kukidhi mahitaji yake ya matumizi na pia kupunguza madeni ya kigeni.

Kamati ya bajeti katika ripoti yake ya mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2019-20 ilipendekeza kwamba shilingi milioni 100 zipewe Chuo Kikuu cha Bomet kwa ujenzi wa kitengo cha afya.

Nyeri haikuwachwa nyuma baada ya shilingi milioni 30 kupendekezwa kwa ujenzi wa hospitali katika eneo la Kiyawara, barabara mjini humo za thamani ya shilinhi milioni 20 na miundo msingi katika taasisi ya KMTC huko Othaya kwa kima cha shilingi milioni 20.

Huko Laikipia, wakaazi waliwafurahisha wabunge kwa kupendekeza shilingi milioni 50 kwa ujenzi wa daraja mbili na ukarabati wa barabara ya Nanyuki-Doldol huku Laikipia Magharibi na Laikipia Mashariki zikipata shilingi milioni 25 kwa uchimbaji visima.

Wakaazi wa Trans Nzoia walipendekeza kukarabatiwa kwa miundo msingi katika chuo cha Anwai cha Kitale ambapo kamati hio ilipendekeza ipewe shilingi milioni 100.