Henry Rotich

Kaza mkanda, hali ngumu kiuchumi yaja, bajeti ya kitaifa yapunguzwa

Kamati ya Bunge ya bajeti imeidhinisha makadirio ya matumizi ya pesa za serikali kipindi  cha mwaka 2019-2020 baada ya kuafikiana na wizara ya fedha katika mazungumzo yaliofanyika siku ya Jumanne.

 

Sarafu za Kenya
Sarafu za Kenya

Kuidhinishwa kwa makadirio hayo ni afueni kuu kwa waziri Henry Rotich ambaye anatarajiwa kusoma bajeti hiyo Juni tarehe 13.

Mwanafunzi aliyetoweka wa shule ya St Stevens apatikana Kawangware

 

Rotich na katibu wa kudumu wa fedha Kamau Thugge walikuwa mbioni siku ya Jumanne kushawishi kamati ya bunge katika juhudi za mwisho kupata maafikiano kuhusiana na bajeti ya kitaifa.

 

parliament

Maafikiano hayo yalijumuisha marekebisho katika makadirio ya bajeti huku baadhi ya idara zikipunguziwa fedha na baadhi ya mipango ya serikali ikiwekwa kando.

 

Saumu Ameona! Patana na Bibi Mrembo wa Seneta wa Lamu Anwar Loitiptip

Rotich aliweza kujiongezea shilingi bilioni 78 zaidi kuliko ilivyokuwa imewekwa katika makadirio ya awali.

 

 

Nyongeza hiyo itagharamiwa na matarajio kuwa serikali itaongeza patio lake hadi shilingi bilioni 35 kufikisha kiasi cha fedha zinazotarajiwa kukusanywa hadi shilingi trilioni 2.1.

 

Peter Crouch amuita mwanawe Divock

Kamati hiyo chini ya uwenyekiti wa mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa inawasilisha ripoti hiyo bungeni leo ili ipate idhini ya katriban wabunge 349.

Mbunge Kimani Ichung'wa na Jaji Mkuu David Maraga
Mbunge Kimani Ichung’wa na Jaji Mkuu David Maraga

 

Hatua hii itampa ruhusa waziri Rotich kusoma bungeni bajeti ya kitaifa kwa kipindi kijacho cha matumizi ya pesa za serikali Alhamisi wiki ijayo.

 

 

Katika ripoti hiyo kamati ya bajeti ilisema walilazimika kuifanyia ukarabati bajeti hiyo kutokana na changamoto za matarajio ya ukuaji wa uchumi wa taifa.

 

 

Kulingana na makadirio hayo, bajeti za Bunge, serikali na mahakama ni jumla ya shilingi trilioni 3.02.

Henry Rotich

 

Hii anamaanisha bajeti ya mwaka huu imepunzwa kwa takriban asilimia 4.2 ikilinganishwa na kipindi cha kifedha cha mwaka uliyopita.

 

 

Serikali ya kitaifa imetengewa shilingi trilioni 1.84, serikali za kaunti zitapokea shilingi bilioni 371.6, bunge litapokea bilioni 43 huku idara ya mahakama ikipokea shilingi bilioni 18.8.

 

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments