Kazi kwa Wazee : Kutana na maajuza wanaofanya kazi ya ukahaba Nyeri

kahaba 1
kahaba 1
Ungelidhani umeyaona na kuyasikia yote lakini makubwa na hata mazito zaidi yapo njiani. Awali ukahaba ulizingatiwa kuwa kazi ya  mabarobaro  lakini huko nyeri nyanya  wa umri wa juu pia sasa wanaiuza miili yao  na hawajutii uamuzi wao

Wanawake hao wanaoshi katika eneo la Chaka  wametegemea kazi hiyo kama njia ya kujipa kipato  ili kujikimu na pia kuwasaidia wajukuu wao ambao waliachiwa na wanao. Wakizungumza katika mahojiano na Runinga ya Mt Kenya TV,  wanawake hao wamesema  kwamba hali ngumu ya  maisha imewalazimu kujiingiza katika biashara hiyo .

Esther  wanjiku  (sio jina lake halisi) hufanya kazi katika mgodi wa mawe lakini giza linapofunika ardhi basi kazi yake papo hapo inageuka na kuwa ya ukahaba. Nyokabi mwenye umri wa miaka  70 (sio jina lake halisi )  anasema licha  ya kazi hiyo kudharauliwa na wengi, imempa  mkate wake wa kila siku .

 HAPO AWALI NINGEJAZA LORI KWA MAWE  KWA WIKI MOJA NA NINGETUMIA NGUVU NYINGI. KWA SASA SINA NGUVU ZAIDI. KILA SIKU LAZIMA NINYWE  POMBE YA SHILINGI 50  KABLA YA  KWENDA NYUMBANI. NINA WATOTO WATANO NA BINTI YANGU ANA WATOTO WATATU

  Alivyoulizwa jinsi wanavyowashughulikia wateja wake, Nyokabi anasema;

 Mnaafikia makubaliano yatakayokuwezesha kupata  unga na pesa. Wakati mwingine anaweza kukupa hata shilingi 200 kwa sababu wengi pia hawana pesa nyingi.

Kabla ya kwenda kuwahudumia wateja wake, Nyokabi hupitia katika eneo la burudani ili kupata kileo cha ‘kumtuliza’ .

Juliah Wambui ( sio lake halisi )  pia anaishi Nyeri na amekuwa kahaba kwa miaka 20 .

Kulingana naye, yeye na wateja wake hawana pesa za kwenda kupata vyumba au danguro na hivyo basi wanamaliza shughuli zao katika vichaka au maeneo mengine ya wazi .

 ‘ Mimi huwahudumia wanaume wa umri wangu. Tunatumia uwanja huu ambao upo mbali ili kupeuka kuonekana na watu. Wakati ninaposikizana na wateja wangu , siitishi pesa kanza, mimi huitisha bia kwanza hata hivyo nahakikisha kwamba silewi. Watu wengi hupenda kufanya mapenzi chini kwenye majani na mkimaliza shughuli zenu, kila mtu anaenda zake. Ninapofika nyumbani naoga  na kisha kutoka tena kumtafuta mteja mwingine .

Julia  anasema yeye hutumia kinga  kwani hataki kuambukizwa maradhi .

 Mimi hurejea katika eneo tofauti la burudani kutafuta mteja mwingine. Nahakikisha kwamba natumia mpira wa kondomu. Nina mipira ya kondomu katika nyumba yangu . Singependa kujua wajukuu wangu wajue ninafanya kazi gani. Wamejaribu kuniuliza mimi huenda wapi nyakati za usiku lakini Sijawaambia .