Kazi lazima ifanywe,'Tanasha kusema atafanya kazi na Diamond hata baada ya kumtema

Baada ya kumtema msanii wa bongo Diamond, Tanasha amefunguka na kusema kuwa ataendelea kufanya kazi na miradi nyingi na aliyekuwa mpenzi wake.

Wawili hao waliachana tu baada ya kutoa kibao cha'gere' pamoja huku Tanasha akiondoka nchini Tanzania na kurudi humu nchini.

Baada ya muda, mama yake Diamond alimiliki gari lililokuwa la Tansha huku wengi wakimkashifu kwa kitendo hicho.

Akiwa katika mahojiano, Tanasha aliulizwa kama anaweza kufanya kazi na aliyekuwa mpenzi wake na alikuwa na haya ya kusema.

"AS AN ARTIST 3-4 YEARS FROM NOW IF WE ARE IN THE SAME SPACE MENTALLY —I HAVE TO RELATE TO AN ARTIST TO WORK WITH THEM—THEN WHY NOT?
WE ARE LIVING IN A FEMALE ERA. IN A CONSCIOUS ERA. WOMEN ARE BEING ELEVATED ESPECIALLY IN THE MUSIC INDUSTRY." Tanasha Alieleza.

Tanasha Donna alipitia mengi alipokuwa mchumba wa Diamond bali alijipa nguvu na kwa hakika amefanya mambo kadhaa tangu aachane na staa wa bongo.

Alipoulizwa kama ataweza kurudiana na Diamond endapo nafasi itakuwa alisema,

"AT THIS POINT, MY MIND HAS BEEN TRAUMATISED TO THE POINT I DON’T KNOW IF I COULD." Alizungumza.