Jacque Maribe na Jowi

”Kazi ya Jowie ilikuwa kumpeleka Maribe kazini na kulala” Binti afunguka

Katika kesi inayoendelea ya Jowie na binti Maribe kuhusu mauaji ya binti Monicah,binti mmoja aliyekuwa mfanyikazi wa Terryanne Chebet alijitokeza kama shahidi kortini na kusimulia yaliyotendeka.

Binti huyu alimfanyia kazi Terryanne kwa zaidi ya miaka mitano na baada ya Terryanne kufutwa kazi kwenye runinga ya Citizen, akaenda kumfanyia kazi Jacque Maribe.

Mungu ni mwema! Huenda mkamuona Jacque Maribe kwenye runinga karibuni

Binti huyu jina lake Pamela alisema kuwa katika nyumba ile ya Jacque walikuwa wanaishi watu watatu, yaani Jacque, mtoto wake na yeye lakini mwaka wa 2018 Jowie alihamia kwake na wakaanza kuishi pamoja.

Vilevile, Pamela alifunguka na kusema kuwa siku moja aliona bunduki ile na alipomuuliza Maribe sababu ya mchumba wake kuwa na bunduki,Jacque alisema kuwa Jowie ana bunduki kwa sababu ya kazi yake kama askari wa jeshi

Step by step:Mwanahabari Maribe alikuwa na Sonko wakati Monica alipouawa-Shahidi

Vilevile,aliambia korti kuwa kazi yake Jowie ilikuwa kumpeleka Jacque Kazini kila siku,kumchukua baada ya kazi na kurudi na kulala.

”Kazi ya Jowie ilikuwa kupeleka Jacque kazini,kumchukua na kulala.”Pamela alisema.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments