KCSE 2019: Orodha ya shule 10 bora zilizojizolea alama ya 'A'

KCSE (1)
KCSE (1)
Waziri wa elimu George Magoha alitangaza matokeo ya mtihani wa KSCE siku ya jumatano.

Jumla ya wanafunzi 627 walijizolea alama ya 'A' katika mtihani huo, ikilinganishwa na 315 mwaka jana, waziri wa elimu George Magoha amesema.

Ifuatayo ni orodha ya shule ambazo zilijozolea alama nyingi za 'A'

Kenya High School - 76

Kapsebt High School - 49

Alliance High School - 48

Moi Kabarak - 30

Alliance Girls - 27

Mary Hill - 25

Maseno School - 25

Nairobi School - 23

Mang'u High School - 23

Moi Girls Eldoret - 21

Mwanafunzi bora ni Tony, kutoka Shule ya Upili ya Kapsabet ambaye alijizolea gredi ya A yenye alama 87.159.

Baraza wa shule ya upili ya Kenya High alijizolea gredi A yenye alama 87.087.

Kaboge Odhiambo kutoka shule ya upili ya Kapsabet alipata gredi A na alama 87.080, Antony Owuor alipata A ya alama 87; Natasha Wawira wa Kenya High alipata gredi ya A ya alama 86.9.