‘KDF walijificha ‘ kichakani wakati wa shambulizi la Manda Bay-Amerika yasema

Manda
Manda
  Wamarekani wamewakosoa wanajeshi wa KDF kuhusiana na mienendo yao wakati wa shambulizi la al shabaab katika  Camp Simba huko manad bay  januri tarehe 5 . Kulingaana na gazeti la the ,  wanajeshi wa Kenya walijificha kwenye majani  wakati wa shambulizi hilo lilopelekea kuuawa kwa  wamarekani  watatu .

" wanajeshi wengi wa Kenya waliopewa jukumu la kuilinda kambi hiyo walijificha kwenye nyasi wakati  wanajeshi wa marekani na  wafanyikazi kadhaa walipokuwa katika mahema yao wakingoja vita kutamatika’ gazeti ya NYT limeandika . Ufichuzi huo henda ukazua lalama kutoka kwa serikali  ya Kenya na KDF kwa  ajili ya  athari zake kuwachafulia sifa na jina wanajeshi wa humu nchini . Mwanajeshi  mmoja wa  Amerika   na raia wawili waliokuwa wanakndarasi waliuawa katika shambulizi hilo la al shabaab .

Wanajeshi wengine wawili wa Marekani walijeruhiwa katika shambulizi hilo . Gazeti hilo la  Amerika pia limeonekana  kuashiria kwamba huenda wafanyikazi wa kenya katika kambi hiyo waliwasaidia wapiganaji wa Al shabaab . Gazeti hilo limesema Kenya ilitangaza kuwakamata washukiwa sita wa al shabaab lakini baadaye ilibainika kwamba walikuwa wapita njia ambao baadaye waliachiliwa huru .