Raila amesema keki ya kitaifa imekuwa ikipungua huku akionya kwamba huenda pakatokea janga endapo hakuna kitakachofanywa ili kuhakikisha kwamba kila mkenya anapata raslimali a kujiendeleza hasa katika kaunti zote 47 .
“ Wananchi wetu na viongozi wanafaa kukugundua kwamba kuzidisha uzalishaji ni jambo muhimu la kuhakikishja kwamba keki ya kitaifa inamfikia kila mmoja ili kuboresha hali ya maisha ya kila mkenya ,hakuna kingine kitakachofaulu’ Odinga amesema kupitia taarifa .
“ Kiwango cha keki ya kitaifa kimekuwa kikipungua kila mwaka ilhali idadi ya watu wanaoingoja imekuwa ikiongezeka .Ndio kwa sababu kugawana shilingi bilioni 316 kw akaunti 47 ni tisho kwa uthabiti wan chi yetu na umoja.’
Raila amesema magavana wanafaa kuhakikisha kwamba kuna uzalishaji wa kutosha katika kaunti .
“ Tunafaa kuona ushirikiano wa vitengo vyote viwili vya serikali kutathmini masuala kama ya kodi ili hatua hiyo iweze kuvutia uwekezaji na biashara na sio kuzuia ukuaji huo hasa katika maeneo ya mashinani’
Raila pia amelalamikia alichotaja kama kutengwa kwa wakulima wadogo wadgo ambao huchangia ustawi wa uchumi wa maeneo ya mashinani .