Kenya haitanunua vifaa vya kuwakinga wahudumu wa afya -Mutahi asema

unnamed (27)
unnamed (27)
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kuwa Kenya haitanunua vifaa vya kuwasaidia wahudumu wa afya nchini almaarufu PPEs baada ya serikali kuanza kutengeneza vifaa hivyo kutoka kwa kampuni za humu nchini.

Akitoa takwimu za kila siku kwa taifa Mutahi amesema kuwa  kampuni za humu nchini zimeanza kutengeneza vifaa hivyo takriban 25000 kila siku.

Kulingana na Mutahi ,vifaa hivyo vya PPEs vilivcyokuwa vimenunuliwa na serikali havikua vimeafikia viwango kamli vilivyokuwa vinavyohitajika.

"The PPEs that are manufactured locally are superior to the PPEs that were being imported before. Our local manufacturers are now able to produce better and quality PPEs", amesema Kagwe.

Amesema baadhi ya vifaa hivyo vimekuwa vikiweka maisha ya madaktari na wahudumu wengine hatarini .

Aliongezea kuwa wizara haitavumilia kuona maisha ya wahudumu wa afya kuendelea kuteseka kwa kutumia vifaa ambavyo havijahitimu viwango.

" We are not going to allow our doctors to be exposed. We will not accept any materials that the doctors themselves are not comfortable with. So people will not just come with any type of PPEs and expect us to accept", alisema Mutahi