Kenya yafikisha watu 126 walioathirika na virusi vya Corona -Asema Waziri Kagwe

mum
mum
NA NICKSON TOSI

Visa vya watu walioathirika na virusi vya Corona katika taifa la Kenya vinaendelea kuongezeka kila siku na kufikia sasa, waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kuwa watu 4 zaidi, wakenya 3 na mpakistani 1 wamepatikana na virusi hivyo baada ya kufanyiwa vipimo vya matibabu na kufikisha idadi kuwa 126.

Watu 672 wangali wanaangaziwa hali yao na serikali baada ya kujumuika na wale walioathirika .

Kati ya watu hao 4 waliothibitishwa kuwa na virusi, 2 waliombukizwa virusi hivyo nchini.

Watu wengine 1781 wanaendelea kutafutwa na serikali baada ya kujumuika na watu walioathirika.

Sampuli za watu takriban 372 wamefanyiwa vipimo vya matibabu chini ya masaa 24.

Wakati uo huo Mutahio ameongeza makata ya watu kuingia kwa nyumba zao kugfikia saa 7 jioni kwa siku nyingine 14 zaidi na kutaka wananchi kudshiriukiana na serikali pamoja na maafisa wa polisi.

Kwa mara nyingi tena waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe amewataka vijana nchini kushirikiana na serikali katika jitihada za kupambana na virusi vya Corona ambavyo vimebisha hodi na kuathiri watu 122 kufikia sasa.Mutahi amesema kuwa taifa la Kenya limejaaliwa idadi kubwa ya vijana ambao wanaratibiwa kuwa viongozi swa kesho na hivyo kuna haja ya kufanya kasi pamoja na serikali .

Akitoa hotuba  yake ya kila siku ,Mutahi pia ametuma risala za rambi kwa jamaa ,ndugu ,marafiki na familia ya Rubani wa shirika la ndege la Kenya Airways Daudi Kimuyu Kibati na kumtaja kama mtu aliyefanikisha kuokoa maisha ya maelfu ya wakenya waliokuwa wanataka kurejea nchini kutoka mataifa yaliyoathirika na Corona.

Mutahi pia amesema kuwa watu 20 ,wametengwa katika hospitali kuu ya Kenyatta wakisubiri kufanyiwa vipimo vya matibabu na madaktari.

Wakati uo huo ameongeza kuwa watu wengine 2000 wamewekwa katika vyumba tofauti wakisubiri kuangaziwa na maafisa wa serikali.