Kenya yakanusha madai ya ndege yake kuzuiwa kutua Tanzania

UHURU MAGUFULI
UHURU MAGUFULI
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni siku ya Jumanne ilikanusha madai kuwa ujumbe wa Kenya uliokuwa umeenda kuhudhuria hafla ya mazishi ya rais mustaafu wa Tanzania marehemu Benjamin Mkapa ulirejeshwa Nairobi na mamlaka nchini Tanzania kabla hata ndege yao kutua.

Habari zaidi;

Ndege hiyo iliokuwa imebeba seneta wa West Pokot Samuel Poghisio ambaye ni kiongozi wa wengi katika seneti, ilirejea mjini Nairobi punde tu ilipofika eneo la Monduli nchini Tanzania, jarida The Citizen liliripoti.

Ripoti hizi hata hivyo zilithibitishwa na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Tanzania Palamagamba Kabudi aliyesema kwamba walitarajia mjumbe wa rais Kenyatta.

Akiwatambulisha wageni katika hafla hiyo ya marehemu Mkapa katika uwanja wa Uhuru, Kabudi alisema kwamba ndege iliokuwa imembeba mwakilishi wa rais Kenyatta, Samuel Poghisio ilikuwa imelazimika kurejea Kenya kabla ya kutua kutokana na hali mbaya ya anga.

Habari zaidi;

“Tulitarajia kuwa naye mjumbe maalum wa rais Uhuru Kenyatta, seneta Samuel Losuron Poghisio...lakini tumepokea ujumbe kwamba ndege alimokuwa ililazimika kurejea Kenya ikiwa hewani. Habari tulizonazo ni kwamba ndege hiyo inatarajiwa kutua salama mjini Nairobi,” Kabudi alisema.

Kauli ya wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Kenya ilikubaliana na ile ya mamlaka nchini Tanzania.

“Lilikuwa tatizo la kiufundi, kwa hivyo Kenya iliwakilishwa na balozi Dan Kazungu. Anahudhuria hafla hiyo ya mazishi,” mkuu wa mawasiliano ya umma Jane Kariuki alisema kwa simu.

Paliibuka madai kuwa huenda serikali ya Tanzania ilihamakishwa na matamshi ya rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumatatu kuhusu utepetevu wa baadhi ya nchi katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza katika hotuba yake ya 10 kwa taifa kuhusu maambukizi ya covid-19, rais Kenyatta aliambiwa wakenya kutopumbazwa na baadhi ya nchi ambazo zimedinda kutangaza takwimu za corona wakidhani kwamba nchi hizo zimefaulu katika kudhibiti maambukizi ya maradhi hayo.

Habari zaidi;

Uhuru alikaribia kutaja Tanzania ambayo imelaumuiwa kwa kukataa kutoa takwimu za maambukizi ya corona na hata kudhibiti matangazo yanayohusiana na janga la corona.

Mara ya mwisho Tanzania kutoa takwimu za corona ilikuwa Aprili 29, ambapo visa vipya 480 vya maambukizi vilitangazwa huku watu 21 wakifariki.