Kenya yakuwa nchi ya tatu kuzindua chanjo ya malaria

Malaria ni ugonjwa unao waua watoto wengi sana walio chini ya miaka tano. Amini usiamini, malaria humuua mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili.

Hata hivyo, jambo la kufurahisha, nchi yetu ya Kenya imeanza kuwapa watoto wachanga chanjo ya malaria ili kupunguza visa vya vifo vya watoto nchini.

Nchi za Africa kama Ghana na Malawi ndizo zilizo kuwa za kwanza kuanzisha mradi huu na kenya ikafuata. Mradi huu umeanzishwa katika kaunti ya Homabay na Kenya inapanga kueneza chanjo hizo kwa kaunti zote.

Zaidi ya hayo, Malaria iliambukiza watu karibu milioni 219 mwaka wa 2017 na kuwaua watu 435 000 wengi wao wakiwa watoto wa kutoka nchi maskini zaidi Africa

Hata hivyo, watu wengi wako kwenye hatari ya kupata ugonja huu, kwa hivyo ni  sharti kila mtu ahakikishe kuwa mtoto wake amepewa chanjo hii ili tupunguze vifo vya watoto kama nchi.