Kenya yaongoza Africa kwa utumiaji wa madawa haramu

Kenya imeorodheshwa katika nafasi ya tatu kwa kuwa taifa lenye udanganyifu wa hali ya juu dunia kote huku likiwa na wanariadha 41 waliozuiwa kukimbia kutokana na utumiaji wa madawa ya  kusisimua misuli.

Kulingana na habari iliyotolewa na kampuni ya AIU Kenya ilitoa wariadha wengi huku Russia 87 na India 42 yakiwa mataifa yanayoipiku Kenya kwa wariadha kutumia madawa ya kusisimua misuli.

Kenya ilijipata katika hali tatanishi baada ya kuleta wakimbiaji waliopatikana na hatia ya utumiajia wa madawa haya ya kusisimua misuli. Jambo hilo lilipelekea Kenya kupewa onyo na shirika la WADA, (World Anti-Doping Agency). Kufuaia maonyo hayo,Kenya iliunda kamati ya kupambana na muasala ya utumiaja wa madawa baina ya wanariadha.

Taifa la Urusi linaloongoza kwa visa vingi vya udanganyifu duniani kote lilipigwa marufuku na shririkisho la WADA kutopata usaidizi wowote.

Kwenye orodha hio ya WADA, kunao wanaume 24 huku wanawake wakiwa 17. Pia kwenye orodha hio ni maafisa wakuu wa riadha humu nchini wakiwemo Mike Kosgei pamoja na Daniel Ayiemba .

Madawa yanayotumiwa sana na wakenya ni pamoja na;Blood booster Erythropoietin- EPO ambayo huchangamsha damu huku ikiongeza hewa ya oxigeni mwilini, Norandrosterone,Prednisone, Salbutamol na Steroids.

Wanariadha kumi walipatikana na Norandrosterone huku wengine wawili wakipatikana na steroids.

Mataifa mengine yaliyoko kwenye orodha hio ni pamoja na; Morocco 30, China 28, USA 17 pamoja na Ethiopia ikiwa na 12.

Kenya inaongoza Africa ikiwa ikifuatwa na Morocco. Siku ya Alhamisi, ADAK ilisema kuwa itaunga mkono upigaji marufuku wa utumiaji wa madwa ndani ya riadha huku shirikisho la Riadha Kenya likiunga mkono hatua hio.