Hii ni kutoka sampuli 1,108 zilizopimwa na kufikisha jumla ya sampuli 59,260 hadi kufikia sasa
Mgonjwa zaidi ameaga dunia na kufikisha 51 watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo hadi kufikia sasa .
kati ya visa hivyo 22 17 ni wanaume ilhali 5 ni vya wanawake . Wagonjwa walioathiriwani kati ya umri wa miaka 24-73.
katika visa hivyo vya leo Nairobi (10), Mombasa (9), Kwale ( 1), Nakuru (1), Taita Taveta(1).
katibu wa utawala wa wizara ya Afya Rashid Aman amesema watu wengine watatu wameruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha 383 idadi ya watu waliopona ugonjwa huo .
Aman amewashauri wakenya kuendelea kutii maagizo yaliyotolewa na wizara ya afya ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi hivyo .Amewapongeza wakaazi katika maeneo yalio chiniya maagizo ya kutotoka nje kwa kushirikiana kikamilifu na serikali .Pia amewahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi ili kupimwa virusi vya corona