Kenya yashinda kiti katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kura 129

unsc
unsc
Kenya  imeshinda kiti cha uanachama katika baraza la usalama la umoja wa mataifa  baada ya kupata kura 129 katika raundi ya pili ua upigaji kura dhidi ya Djibouti.

Djibouti  ilipata kura 62 katika raundi ya pili baada ya kuinyima Kenya ushindi katika raundi ya kwanza siku ya Jumatano.  Siku ya Jumatano Kenya ilipata kura 113 dhidi ya 78 za Djibouti  na ilihitaji kura 128 ili kupata ushindi wa moja kwa moja kati ya kura 192 za mataifa wanachama

Hatua hiyo ililazimu bunge la  mataifa wanachama kuitisha awamu ya pili ya upigaji kura ili kuamua mshindi kati ya Kenya na Djibouti  kumtafuta mwakilishi wa Afrika katika baraza hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kenya inaichukua nafasi ya Afrika Kusini  na itahudumu kuanzia mwaka wa 2021 hadi 2022. Nairobi sasa inajiunga na India, Mexico, Norway  na  Ireland  kuwa miongoni mwa wanachama wasio wa kudumu wa baraza hilo ambao ni (Russia, China, UK, US, France) kupitisha maazimio ya kudumisha amani na usalama duniani wakati wa kipindi cha mwaka wa 2021/2022.