Kenya yashuka hadi nafasi ya 5 katika ubingwa wa dunia - Doha Qatar

NA NAOM MAINYE

Winny Chebet, Faith Kipyegon, Ronald Masagala,Ronald Cheruiyot na George Wafula walifuzu kwa fainali za mbio za mita 1500 kwenye mbio za ubingwa wa dunia mjini Doha-Qatar.

Kwenye jadwali Marekani inaendelea kuongoza katika mashindano hayo kwa kuwa na jumla ya medali 18, nane za dhahabu, nane za fedha na mbili za shaba huku Kenya ikishuka hadi nafasi ya tano kwa kuwa na medali nne pekee, mbili za dhahabu na mbili za shaba baada ya Uchina, Jamaica na Great Britain kutwaa nafasi za pili, tatu na nne wakiwa na jumla ya medali 9,6 na 3 mtawalia. Mashindano hayo yatakamilika Jumapili 6/10/2019.

Katika mechi ya Europa, Arsenal waliilaza Standard Liege mabao 4-0 katika mchuano wa kuwania taji la ubingwa Barani Uropa, mabao yaliyofungwa na wachezaji Garbriel Martinelli,Joseph Willock na Daniel Ceballos katika dakika za 14,16,22 na 41 mtawalia ugani Emirates.

Arsenal walionekana kuimarika baada ya sare ya 1-1 dhidi ya manchester United katika mechi ya ligi ya primia siku ya Jumatatu. Roma walitoka sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji kutoka Australia Wolfsberger AC ugani Merkur Arena huku masaibu ya Machester United yakiendelea kwa kutoka sare tasa dhidi ya wenyeji AZ Alkmaar ugenini Cars Jeans Stadion.

Man United haijasajili ushindi ugenini tangu Machi mwaka huu walipolaza PSG katika mchuano wa kuwania taji la ubingwa Barani Ulaya. Kocha wa Machester Ole Gunner Solsker alielezea kufurahishwa na wachezaji wake na kusema kwamba walistahili kushinda mchuano huo na kudai kwamba walinyimwa penalti.